Back
Explore every episode of the podcast SBS Swahili - SBS Swahili
Dive into the complete episode list for SBS Swahili - SBS Swahili. Each episode is cataloged with detailed descriptions, making it easy to find and explore specific topics. Keep track of all episodes from your favorite podcast and never miss a moment of insightful content.
| Title | Pub. Date | Duration | |
|---|---|---|---|
| Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaendelea kukabiliana na shinikizo lakutangaza msimamo wayo kwa viwango vya uhamiaji nchini | 11 Sep 2026 | 00:14:00 | |
Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji. | |||
| Makala Leo:Tunachojua kuhusu usalama wakimataifa miaka 25 baada ya tukio la 9/11 | 11 Sep 2026 | 00:12:34 | |
Ni miaka 25 tangu karibu watu 3,000 waliuawa katika mashambulizi ya Septemba 11, ambayo yalisababisha Vita dhidi ya Ugaidi vilivyoongozwa na Marekani na kuiingiza Australia katika vita nchini Afghanistan na Iraq. | |||
| Mumbi afunguka kuhusu mapokezi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia | 11 Sep 2026 | 00:05:43 | |
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba. | |||
| Taarifa ya Habari:Upinzani wa mseto waomba maelezo zaidi kabla ya kura ya mageuzi ya sheria za mitandao ya kijamii zilizo imarishwa | 08 Sep 2026 | 00:13:21 | |
Makampuni ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwapa watumiaji chaguo la kuzima algoriti yao, chini ya rasimu za sheria zilizopangwa kufichuliwa na serikali wiki hii. | |||
| Yaliyojiri Afrika:Agizo la Rais Ruto lazua hofu miongoni mwa wahamiaji wenye asili ya Burundi | 08 Sep 2026 | 00:08:54 | |
Nchini Kenya, ukosoaji umekuwa ukiongezeka tangu tangazo la Rais William Ruto Jumatano iliyopita. Alisema kwamba biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wageni nchini Kenya lazima zifunge kuanzia Jumatatu, Septemba 7. | |||
| Makala Leo: Unachohitaji kujua kuhusu magonjwa ya msimu huu wa masika | 08 Sep 2026 | 00:13:16 | |
Australia inapo ingia katika majira ya kuchipua, wataalamu wanawasihi watu wasiache kujilinda dhidi ya magonjwa ya msimu. | |||
| Taarifa ya Habari:Sera ya malipo ya uzeeni ya One Nation yakosolewa vikali | 07 Sep 2026 | 00:04:57 | |
Chama cha One Nation kina kana kwamba sera yake mpya ya malipo ya uzeeni itasababisha uondoaji mkubwa wa malipo ya uzeeni, au kuongezeka kwa mfumuko wa bei. | |||
| Mumbi afunguka kuhusu maandalizi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia | 02 Sep 2026 | 00:12:18 | |
Wanachama wa Jumuiya za Afrika wanao ishi jijini Sydney, New South Wales wana jiandaa kuhudhuria tamasha maalum. | |||
| Makala Leo: Dunia yamkumbuka gwiji wa muziki Dolly Parton | 28 Aug 2026 | 00:09:05 | |
Gwiji wa muziki wa Country, Dolly Parton, amefariki akiwa na umri wa miaka 80. | |||
| Yaliyojiri Afrika: CCM yamtimua Dkt Emmanuel Nchimbi | 28 Aug 2026 | 00:07:51 | |
Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM umemvua uanachama Emmanuel Nchimbi na kumpitisha Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kujaza nafasi ya Makamu wa Rais. | |||
| Taarifa ya Habari:Australia yatoa kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal | 28 Aug 2026 | 00:14:52 | |
Serikali ya Australia inaanzisha kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal, huku idadi ya Waaustralia waliopotea ikiongezeka hadi 39. | |||
| Makala Leo:Kwa nini baraza lamawaziri wakitaifa haliku gusa vituo vya mbadala vya data | 28 Aug 2026 | 00:10:13 | |
Mkutano wa viongozi wa shirikisho, majimbo na wilaya ulimuacha Waziri Mkuu Anthony Albanese akikubali agizo la vituo vya data vinavyoweza kutumika tena. | |||
| Makala Leo:Wa Australia 34 miongoni mwa watu ambao wamepotea katika mafuriko Nepal | 28 Aug 2026 | 00:11:48 | |
Takriban watu 160 wameuawa, na mamia wakiwemo watalii na Waaustralia 34 hawajulikani walipo, kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea kwenye mpaka wa Nepal na Tibet. | |||
| Taarifa ya Habari:Makumi yawa Australia hawajulikani waliko katika mafuriko nchini Nepal | 27 Aug 2026 | 00:05:09 | |
Waziri Mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa Waaustralia 34, hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa ya ghafla kwenye mpaka wa Nepal-Tibet. | |||
| Yaliyojiri Afrika:Ujumbe maalum wafuatilia usitishaji mapigano DRC | 25 Aug 2026 | 00:07:33 | |
Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda. | |||
| Taarifa ya Habari:Hospitali za New South Wales kupewa nafasi zaidi za matibabu | 25 Aug 2026 | 00:14:24 | |
Hospitali za New South Wales zitapata nafasi zaidi za matibabu za muda mfupi ili kupunguza shinikizo kwa idara za dharura. | |||
| Makala Leo: Mrundikano wa visa za wenza unao waacha waaustralia katika sintofahamu | 25 Aug 2026 | 00:08:38 | |
Mchakato mpya wa kipaumbele ambao unaweza fanya baadhi ya raia wa Australia, wasubiri kwa muda mrefu zaidi kwa wenzi wao kupokea visa umesababisha ukosoaji. | |||
| Makala Leo:'Usibofye kitu chochote':Jinsi barua pepe moja inavyoweza haribu biashara | 25 Aug 2026 | 00:07:34 | |
Waaustralia wanapoteza mamia ya mamilioni ya dola kutokana na matapeli, huku matapeli wakizidi kutumia akili mnemba kuwadanganya waathiriwa wao. | |||
| Taarifa ya Habari:Ripoti mpya yaitaka Australia iboreshe usalama wa dawa na itoe wakalimani kwa jamii za tamaduni mbalimbali | 21 Aug 2026 | 00:13:56 | |
Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi. | |||
| Yaliyojiri Afrika:7 wafariki katika ajali ya helikopta Kenya | 21 Aug 2026 | 00:07:17 | |
Watu saba, wakiwemo raia watano wa Marekani na mkuu wa ujasusi wa Ecuador, wamefariki baada ya helikopta ya watalii kuanguka karibu na Mlima Ololokwe, katika kaunti ya Samburu nchini Kenya. | |||
| Makala Leo:Mabadiliko ya NDIS yatakuathiri vipi? | 21 Aug 2026 | 00:12:50 | |
Mamia ya maelfu ya watu watapoteza msaada kutoka NDIS, baada ya mabadiliko yanayolenga kupunguza ukuaji katika mpango huo kupitishwa ndani ya Seneti kwa uungwaji mkono wa Upinzani wa Mseto usiku wakuamkia. | |||
| Yaliyojiri Afrika:Askari pori watuhumiwa kwa mauaji ya raia Tanzania | 18 Aug 2026 | 00:07:52 | |
Kituo cha sheria cha haki za binadamu Tanzania, kime eleza wasiwasi kuhusu madai ya watu kuuawa, kujeruhiwa au kupotea katika maeneo ya hifadhi nchini humo. | |||
| Taarifa ya Habari:Upinzani wa Mseto watishia kuzuia mabadiliko ya NDIS isipokuwa mwanya wa kodi ya mjane utakapofungwa | 18 Aug 2026 | 00:13:56 | |
Upinzani wa Mseto unatishia kuzuia mabadiliko ya serikali kwa NDIS, isipokuwa serikali ya Labor iharakishe sheria ya kufunga kile kinachoitwa kodi ya mjane. | |||
| Makala Leo:Mageuzi ya NDIS yanatarajiwa kuwa sheria ila, wanaharakati wadai makato yata sababisha madhara | 18 Aug 2026 | 00:16:29 | |
Mageuzi ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu yamejadiliwa katika Seneti, huku sheria ikitarajiwa kupitishwa wiki hii kwa msaada wa Upinzani wa Mseto. | |||
| Can you pick fruit from someone's garden? - Australia Yafafanuliwa:Je, unaweza chuma matunda kutoka bustani ya mtu? | 18 Aug 2026 | 00:10:31 | |
Walking through an Australian suburb, you might spot everything from curry leaves and lemons to tomatoes and herbs growing in front gardens or on verges. But is it legal to pick it? This guide explains when it's legal to pick produce, why permission matters, and how community gardens offer another way to grow your own food. - Ukitembea katika kitongoji cha Australia, unaweza ona kila kitu kuanzia majani ya kari na limau hadi nyanya na mimea inayokua katika bustani za mbele au kwenye ukingo. Lakini je, ni halali kuvivuna? Mwongozo huu unaelezea wakati ni halali kuvuna mazao, kwa nini ruhusa ni muhimu, na jinsi bustani za jamii zinavyotoa njia nyingine ya kukuza chakula chako mwenyewe. | |||
| Taarifa ya Habari:Wafanyakazi wa kusambaza vyakula kuongezewa mshahara kuanzia leo | 17 Aug 2026 | 00:05:35 | |
Takriban idadi yawa Australia 250,000 wanaosafirisha vyakula kutoka hotelini na dukani kwa ajili ya kujikimu, wanatarajiwa kupokea mshahara wa chini kisheria kwa mara ya kwanza. | |||
| Makala Leo:Serikali kuwekeza mamilioni katika nyumba za waathiriwa wa unyanyasaji wa majumbani; lakini je, inatosha? | 14 Aug 2026 | 00:11:36 | |
Mgogoro wa makazi ukiendelea, vurugu za kifamilia na majumbani (DFSV) ndio sababu kuu ya wanawake na watoto kuondoka nyumbani kwao na kukosa makazi. | |||
| SBS Learn Eng Ep 117 Jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu | 14 Aug 2026 | 00:15:27 | |
Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu katika maktaba? | |||
| Taarifa ya Habari:Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni | 14 Aug 2026 | 00:15:52 | |
Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni leo. Uchunguzi huo ulizinduliwa katika mwezi Mei ili kuchunguza mapendekezo ya Serikali, ya kuokoa karibu dola bilioni 38 kwa kipindi cha miaka minne. | |||
| Yaliyojiri Afrika: Uganda na Tanzania za zindua ushirikiano wa nishati | 14 Aug 2026 | 00:06:59 | |
Bandari ya Tanga itakuwa kitovu muhimu cha nishati katika jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya ushirikiano mpya wa nishati uliozinduliwa kati ya serikali ya Uganda na Tanzania. | |||
| Makala Leo:Sensa imekwisha ila, bado hauja chelewa kama hauja jaza fomu yako | 14 Aug 2026 | 00:06:49 | |
Sensa ya 2026 imekwisha na idadi kubwa ya Waaustralia walikamilisha utafiti huo mtandaoni. | |||
| Taarifa ya Habari:Serikali yawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama | 11 Aug 2026 | 00:13:24 | |
Serikali inawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama, kufuatia visa vya hivi karibuni vya roboti za AI kufanya ujambazi na uvunjaji wa data katika mashirika makubwa. | |||
| Yaliyojiri Afrika:Wanariadha wa Uganda watoweka Scotland | 11 Aug 2026 | 00:07:58 | |
Mabondia wanne wa timu ya Uganda, wametoweka baada yakufeli kujitokeza kwa safari zao za ndege zakurejea nyumbani, baada ya kushiriki katika michezo ya jumuiya yamadola mjini Glasgow. | |||
| Makala Leo: Watetezi wa ulemavu waomba mlinzi nakuonya kuhusu 'athari kubwa' mageuzi yanapokaribia | 11 Aug 2026 | 00:09:10 | |
Watetezi wa ulemavu wanaihimiza serikali kufikiria upya mabadiliko ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu unao julikana kama NDIS, kabla ya kura ya bunge inayokaribia kuhusu mageuzi yaliyopendekezwa. | |||
| Taarifa ya Habari:Wafanya biashara waomba ushirikiano na serikali kabla ifanye mabadiliko katika uhamiaji | 10 Aug 2026 | 00:06:09 | |
Vikundi vya wafanyabiashara vinaihimiza serikali ya shirikisho kushirikiana nao, katika mashauriano kabla ya mabadiliko yoyote makubwa kutangazwa kuhusu sera ya uhamiaji. | |||
| Taarifa ya Habari:Ofisi ya takwimu ya Australia yahimiza wanao ishi katika nyumba zenye watu wengi wasiwe na hofu kushiriki katika sensa | 07 Aug 2026 | 00:12:52 | |
Usiku wa sensa ukikaribia, maafisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia wanawahimiza watu wanao ishi katika makaazi yenye watu wengi sana, wasiwe na hofu yakushiriki kwa sababu hapatakuwa athari yoyote ya kisheria. | |||
| What are my rights if stopped by police in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Haki zangu ni zipi kama nitasimamishwa na polisi nchini Australia? | 07 Aug 2026 | 00:13:43 | |
Police officers have a range of operational powers they can exercise under legislation, including to ask questions, give ‘move on’ directions and conduct searches. Here’s what you need to know about your basic rights and obligations in a police interaction. - Maafisa wa jeshi la polisi wana mamlaka mbalimbali ya kiutendaji ambayo wanaweza kuyatumia chini ya sheria, ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali, kutoa maelekezo ya 'kutoka ulipo' na kufanya upekuzi. Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu haki na wajibu wako wa msingi katika mwingiliano wa polisi. | |||
| SBS Learn Eng Ep 116 Jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama | 07 Aug 2026 | 00:15:22 | |
Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama? | |||
| Taarifa ya Habari:Mfanyabiashara afariki mjini Melbourne baada ya tukio linalo shukiwa kutekelezwa na wezi | 07 Aug 2026 | 00:05:15 | |
Mfanyabiashara mmoja wa duka mjini Melbourne amefariki baada ya kushambuliwa alipokuwa akijaribu kuzuia kundi la vijana walio kuwa waki iba dukani. | |||
| Yaliyojiri Afrika: DRC yaadhimisha GENOCOST | 04 Aug 2026 | 00:07:38 | |
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ameongoza kumbukumbuku ya mauaji ya GENOCOST jijini Kinshasa, inayofanyika kila tarehe 2 mwezi Agosti. | |||
| Taarifa ya Habari:Mamia ya watu wakimbia mapigano Tigray na kuingia Sudan | 04 Aug 2026 | 00:13:24 | |
Mamia yawa Ethiopia kutoka eneo la kaskazini mwa Tigray, wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Sudan katika siku mbili zilizopita, wakikimbia mapigano karibu na mpaka. | |||
| Makala Leo:Australia inakabiliwa na 'tsunami ya uharibifu' mkubwa kutokana na mlipuko wa virusi vya homa ya ndege H5 | 04 Aug 2026 | 00:11:30 | |
Jimbo la Kusini Australia huenda linakabiliwa na tukio la kwanza la vifo vingi vya wanyamapori nchini Australia linalohusishwa na homa ya ndege ya H5N1. | |||
| Makala Leo:Benki ya Hifadhi yasema wa Australia wengi hawa elewi jinsi viwango vya riba vinavyofanya kazi | 04 Aug 2026 | 00:08:05 | |
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Australia kimepungua, lakini shinikizo la bei la msingi linabaki kuwa juu sana. | |||
| Taarifa ya Habari | 03 Aug 2026 | 00:05:09 | |
Mdhibiti wa ushindani [[ACCC]] ameombwa na serikali ya shirikisho kufuatilia vituo vya mafuta kwa matukio yoyote ya kupunguzwa kwa bei - sasa kwa kuwa punguzo la muda la ushuru wa mafuta limeisha. Visa 74 vya aina ya H-5 ya homa ya ndege vimethibitishwa nchini Australia.Hiyo inajumuisha uthibitisho wa tukio la kwanza la vifo vingi humu nchini kutokana na virusi hivyo Kusini mwa Australia. Mji wa Ceuta mwishoni mwa juma haukuonekana tena kama jiji lililokuwa na wasiwasi, lakini wakazi bado walikuwa wameshtushwa na matukio ya wiki. Wengi wa wahamiaji 60,000 walioingia Ceuta wamerudi Morocco. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili. | |||
| Taarifa ya Habari:Kiongozi wa Victoria, ajiuzulu baada ya siku kadhaa za shinikizo dhidi ya uongozi wake | 28 Jul 2026 | 00:14:42 | |
Jacinta Allan amejiuzulu kama Kiongozi wa Victoria, akisema ni uamuzi sahihi kwa Wa-Victoria. Tangazo hilo limekuja nusu saa tu baada ya changamoto inayotarajiwa ya uongozi katika mkutano uliopangwa wa chama cha wabunge, kuashiria kurudi kwa bunge la jimbo. | |||
| Australia Yafafanuliwa:Tamasha ya Garma ni nini, na kwa nini ni muhimu? | 28 Jul 2026 | 00:10:45 | |
Kila mwaka, maelfu ya watu husafiri kwenda katika jamii ya kijijini kaskazini mashariki mwa Arnhem Land katika Eneo la Kaskazini. | |||
| Makala Leo: Jacinta Allan akataa kujiuzulu, pambano la uongozi wa chama cha Labor cha Victoria likiongezeka kasi | 28 Jul 2026 | 00:11:00 | |
Kiongozi wa Jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema atapambana na changamoto ya uongozi inayokuja baada ya viongozi wa mirengo tafuati ndani ya chama cha Labor, kukutana na kukubaliana kwamba amepoteza uungwaji mkono wa wengi katika mkutano wao. | |||
| Taarifa ya Habari: Kiongozi wa Victoria asisitiza hajiuzulu! | 27 Jul 2026 | 00:05:00 | |
Kiongozi wa jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema hatajiuzulu kutoka wadhifa wake, miezi minne kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo. | |||
| Yaliyojiri Afrika:Kenya yapokea tani 4.5 zavifaa vya matibabu vya Ebola kutoka India | 24 Jul 2026 | 00:07:44 | |
Kenya imepokea shehena ya kwanza ya tani 4.5 za vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali ya India, ili kuimarisha uwezo wa nchi kujiandaa kukabiliana na uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. | |||
| Taarifa ya Habari: Hatua ya Marekani kuongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia yazua ukosoaji | 24 Jul 2026 | 00:13:33 | |
Utawala wa Trump umeongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia kutoka asilimia 10 hadi 12.5, huku kiwango kipya kikianza kutumika alasiri ya leo Ijumaa. | |||
© My Podcast Data · Independent project · Data from Apple & Spotify