Retour

Explorez tous les épisodes du podcast Meza Huru

Plongez dans la liste complète des épisodes de Meza Huru. Chaque épisode est catalogué accompagné de descriptions détaillées, ce qui facilite la recherche et l'exploration de sujets spécifiques. Suivez tous les épisodes de votre podcast préféré et ne manquez aucun contenu pertinent.

Rows per page:

1–24 of 24

TitreDateDurée
Mezani na TAJI "MASTER T" LIUNDI #2303 Jan 202504:13:07

Kama ulishawahi kuisikia ile story ya mtangazaji wa kwanza kucheza wimbo wa Bongo Fleva kwenye radio. Mtangazaji huyo, leo amepata nafasi ya kutubariki na historia yake. Jinsi alivyochangia muziki huu kuwa kimbilio la vijana wengi sana kama sehemu ya ajira yao.

Jina lake kamili ni Taji George Liundi au MASTER T kama alivyobatizwa na Charles Hillary. Kuanzia alivyoanza kutangaza Redio One, moja ya vipindi vyake vya awali kabisa cha DJ Show, kabla ya kuwaachia mikoba wakina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one na kwenda kufanya kazi kwenye media zingine.

Karibu mezani umfahamu zaidi.

Mezani na LUCCI #2201 Nov 202401:53:47

Marehemu CPWAA anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (KING OF BONGO FLEVA CRANK) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na LUCCI chini ya Mawingu Studio. Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank. Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.

Mezani na RAS INNO #1328 Oct 202202:06:05

Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania. 

Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo.

Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae

Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia,

Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu.

#MezaniNaRasInno 

#MezaHuru 

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na CAROLA KINASHA #1221 Oct 202202:17:24

Carola Kinasha, ukimuona huwezi kuamini ana miongo sita duniani. First lady wa Bene Bene na baadaye Shada.

Msomi wa chuo kikuu aliyechagua kufanya muziki kama kazi. Mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa stahiki na haki za utunzi, na moja walioupeleka mbali sana muziki wa asili ya Afrika. Ni mcheshi na mwenye maarifa mengi sana kuhusu maisha na safari ya muziki wetu tangu miaka ya themanini mpaka leo hii.

Unajua kisa chake na Remmy Ongala kilichozaa kibao maarufu cha Karola? Unajua nini maana ya segese?

Unajua kwamba yeye ni mtu aliyekuwa nyuma ya chorus nzuri na tamu za Bongofleva yetu hii? Carola Kinasha ni nyota wa muziki wetu na Almasi inayowaka kama taa. 

Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu

#MezaniNaCarolaKinasha 

#MezaHuru 

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na MIKE TEE #1114 Oct 202201:58:40

Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu. 

Mike Tee alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 90, akiimba kwaya kanisani na taratibu akaanza kujifunza kuandika na kuimba mistari kupitia mashairi ya gazetini baada ya kukutana na Ntwa mmoja wa waanzilishi wa WWA (Wagumu Weusi Asilia).

Amefanya kazi na watayarishaji kama P Funk na Master Jay, amefanya hits na wasanii kama Juma Nature, Q Chief, Mad Ice na Komando Jide

Unajua kuhusu ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya? Mike Tee amenyoosha taarifa. Sitaki kumalizia stori yake. Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu

#MezaniNaMikeTee 

#MezaHuru 

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na UNCLE JOHN KITIME #1007 Oct 202202:17:30

Mzee Kitime ama Ango "Uncle" Kitime kama mwenyewe anavyojitanabaisha kwenye mitandao. Ni mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi kutoka Kilimanjaro Band maarufu kama "Wana Njenje", mmoja wa wanakamati ya kutetea muziki wa dansi na tasnia ya muziki kwa ujumla, Mtangazaji wa Radio, Muigizaji wa Filamu, Mchekeshaji na Mtunza historia ya Music wa Tanzania.

Tumekaa naye na kupata historia ya muziki wake na harakati zake tangu mwaka 1967 hadi leo akiwa na JFK BAND.

Jumuika nasi mezani tumsikilize Gwiji huyu wa Tasnia yetu, Karibu.

#MezaniNaJOHNKITIME 

#MezaHuru 

  • Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
  • Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 
  • Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
  • Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 
  • Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
  • Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 
  • Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
  • Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 
  • YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

  • Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 
  • Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
  • Instagram - https://instagram/mezahurupodcast

Mezani na MASTER JAY Part II30 Sep 202200:58:38

Sehemu ya pili ya maongezi na Master Jay. Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji

Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu

Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁

Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo.

Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu.

#MezaniNaMasterJay

#MezaHuru

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na MASTER JAY Part I23 Sep 202201:26:36

Nani asiyemfahamu Master Jay? Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji

Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu

Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁

Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo.

Jumuika nasi mezani, tusikilize PART I ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu.

#MezaniNaMasterJay

#MezaHuru 

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na BONILUV #TheGodfather Part II16 Sep 202201:19:32

Sehemu ya pili na Kaka Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv. Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa  #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva  Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya Poppaluv 😉 Karibu.  #MezaniNaBoniluv #MezaHuru  

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...  

Applepodcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...  

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...  

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...  

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...     

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...  

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na BONILUV #TheGodfather Part I 09 Sep 202201:17:09

Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa  #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva  Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tumsikilize Poppaluv 😉 Karibu. 

#MezaniNaBoniluv 

#MezaHuru 

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   

Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na DUNGA #0502 Sep 202201:55:00

#MezaniNaDunga

#MezaHuru

#Dunga

Wengi wetu tunamfahamu kwa jina la Dunga ama Mandugu.

Jina lake kamili ni Ambrose Akula Akwabi. 

Huyu ni mtu muhimu sana katika muziki wetu.

Amekuwepo tangu enzi tunajitafuta. 

Dunga na kaka yake (Shakii) wanaunda Mandugu Digital.

Amefanya kazi nyingi sana mashuhuri na nyingine unaweza usiamini anahusika nazo.

Jumuika nasi mezani, tumsikilize Mwamba Huyu 😉

Karibu.

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...

deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...

boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...

youtube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...

facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...

twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na JORS BLESS #0426 Aug 202201:32:28

Johnson Sululu a.k.a Jorsbless ni sehemu ya kizazi bora cha utayarishaji na uandaaji wa midundo katika tasnia ya muziki Tanzania

Amefanya kazi na wasanii kama Mapacha, Rama Dee, Nikki Wa Pili , Adili n.k

Unakumbuka kuhusu ANTI-VIRUS Movement? Tumeligusia hili pia 😁

Amefanya kazi kama DJ katika kituo cha #TimesFm na baadae #AzamTV kama Sound Engineer

Tumekaa na JORS na kupiga soga kuhusu maisha kuanzia mwanzo wa kazi zake hizi mpaka leo hii

Unajua Mwaka 2008 Baba yake mzazi alimpatia kiasi cha shilingi Milioni 2 za Kitanzania ili afungue studio yake?

Jumuika nasi Mezani, Karibu!

Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...

Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...

deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...

boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...

youtube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...

facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...

twitter - https://twitter.com/MezaHuru

Mezani na DARK MASTER #2120 Sep 202401:30:04

Bado kiwanda cha Bongo Fleva kinaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa vijana walioiwakilisha Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2001 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zinachezwa na kusikilizwa mpaka hivi sasa.

Wanaitwa Chemba Squad, ambapo ndani yake majina kama Noorah aka Baba stylz, Dark Master, Albert Mangwea na Mez B wa area C yalitajwa kuunda kundi hilo.

Ngoma kama Ice Cream, Ghetto langu na Kama Vipi zinatajwa kama ngoma bora za muda wote kutoka kwa wakali hao ambapo hivi sasa wamebaki wawili tu (Noorah yupo zake Shy Town na Dark Master akiwa Dar es salaam) huku bahati mbaya Ngwea na Mez B wakiwa ni marehemu (RIP).

Leo tunakusogezea historia kamili na mengi usiyoyajua kuhusu Dark Master aka MwanaChemba.

Mezani na MEJAH #0319 Aug 202201:18:58

MEJAH ni Mwana Hip Hop na Mjasiriamali aliyegeuza mahaba yake ya uchora machata(GRAFFITI), Kusafiri, Kuendesha baiskeli  kuwa sehemu ya kipato chake Tumepata nafasi ya kuzungumza nae na anatupitisha katika historia ya maisha yake kuanzia kuandika sehemu ya wimbo wa JCB wa Kundi la Watengwa,Kuuza majarida mbalimbali mfano "The Source" mpaka kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Graffiti kupitia kundi la Wachata Bila kusahau ni Classmate wa January Makamba 😁 Karibu tumsikilize

"Kwenda Mbele"14 Aug 202200:56:59

A Conversation with Duke Part ii

"The First Session"11 Aug 202200:50:10

First part of Duke opening up about his journey in Tanzanian Music.

#KaribuMezaHuru09 Aug 202200:00:34

A Conversation about Music in Tanzania. From genesis to where it's now. A 20yrs+ journey in the game. Looking at this history from a perspective of our guest. This is Meza Huru, Karibu.

Mezani na FEROOZ #2002 Aug 202401:35:55

Je Unamfahamu FERUZI MRISHO? Gwiji na moja wa waanzilishi na NUNDA mkuu wa DAZ NUNDAZ. Mwenyewe akitambulika zaidi kama Kamanda kabla Kamanda haijawa THE ANTHEM it is now. Leo tuko nae mezani akitusimulia safari yake yote ya mziki, toka anaandikiwa mashairi na dada yake Achane mpaka anatunga tungo matata kama Starehe, Kamanda, Nitafanya Nini, Jirushe, Elimu dunia N.K. Karibu Mezani.

Mezani na MARLON LINJE #1918 Jul 202402:58:42

Je, Unamfahamu producer ambaye, dare I say it, bila yeye labda kwaya au bendi yako maarufu usingeisikia kama ulivyoisikia? Producer ambaye amefanya zaidi ya 80% ya production ya mziki wote wa bendi na kwaya Tanzania kwa miaka 30. Marlon Linje, bonge la mshika dau, leo yupo nawe mezani, karibu.

Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #1825 Nov 202202:30:38
Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo.  nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)?  Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo? Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare 😁 Meza Huru imekaa nao na kupata simulizi ya maisha yao ya muziki na amini kwamba, inavutia sana.  Jumuika nasi mezani kuwasililiza 😊, Karibu  #MezaniNaMandojoNaDomokaya  #MezaHuru
Mezani na KIBACHA Part II22 Nov 202201:41:22

Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha

Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.

Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. 

Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.

Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.

Mwamba huyu hapa 😊

#MezaniNaKBC 

#MezaHuru 

Mezani na KIBACHA Part I18 Nov 202201:39:08

Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha

Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.

Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. 

Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.

Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.

Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa 😊

#MezaniNaKBC 

#MezaHuru 

Mezani na DOLO #1511 Nov 202202:09:20
Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK.  Kutoka maeneo ya TEMEKE.  Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo,  mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK. #MezaniNaDolo  #MezaHuru
Mezani na KR MULLAH #1404 Nov 202201:30:54

KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family

Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi

Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk.

Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo

Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba.

#MezaniNaKakaRashidi 

#MezaHuru

© My Podcast Data