Découvrez des podcasts liées à Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu. Explorez des podcasts avec des thèmes, sujets, et formats similaires. Ces similarités sont calculées grâce à des données tangibles, pas d'extrapolations !
Il n'y a pas de contenu associé à ce podcast.
Aucun lien partagé par ce podcast
Makpandu: Hofu yatanda kwa wakimbizi wa Sudan walio kambini Makpandu Sudan Kusini
vendredi 27 mars 2026 • Durée 02:38
Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS.Kwa muda mrefu kambi ya wakimbizi ya Makpandu imeonekana kuwa kimbilio, lakini sasa imegeuka kuwa eneo la mashaka, na hofu. Bekia Mahadi Ali, mama wa watoto wanane aliyekimbia vita nchini Sudan akitarajia kupata hifadhi, sasa amejikuta akiishi kwa wasiwasi mkubwa baada ya ghasia kuibuka upya katika eneo hili. Furaha ya kupata usalama imetoweka, ulinzi umepungua, Bekia anahofia maisha yake na ya familia yake."Hakuna usalama kabisa hapa kambini na tunaogopa, nilikimbia na wanangu bila baba yao. Watoto hawa ni jukumu langu, tulikuja hapa kutafuta kimbilio lakini hawawezi kwenda shule, sina cha kufanya. Ninachoomba tuhamishwe kutoka kambi hii,”Wakimbizi katika kambi ya Makpandu wanaripoti kuwa watu wenye silaha huingia ndani ya kambi mara kwa mara, wakifyatua risasi hovyo, kuwatishia watu, na kupora au kuchoma moto mali za raia. Omar Ibrahim, ni mkimbizi mwingine kutoka Sudan, anafunguka."Wakati mwingine tunawachukua wanawake na watoto wetu kwenda kulala vichakani kwa sababu hakuna uhakika wa usalama ndani ya kambi. Hatuwezi hata kwenda shambani kulima. Tunaiomba Serikali na Umoja wa Mataifa waingilie kati, tulikimbia risasi nchini Sudan, lakini tumekutana na risasi zilezile tena hapa."Kufuatia shambulio la hivi karibuni lililosababisha kifo cha mkimbizi mmoja wa Sudan, kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kimefanya doria katika kambi hiyo ya Makpandu ili kutathmini hali ya usalama. Thomas Bazawi, ni Afisa wa Ulinzi, Mpito na Urejeshwaji wa UNMISS, anafafnua jukumu lao.“Jukumu letu ni kusaidia kurejesha imani kwa kushirikiana na jamii, mamlaka za mitaa, vikosi vya usalama na wengineo. Tunafanya kazi na wadau wote kuimarisha usalama ili watu waweze kujiamini na kuendeleza maisha yao tena.”Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa uwekezaji katika amani kupitia mpango wa Hatua kwa Ajili ya Kulinda Amani (A4P) ni muhimu kwa usalama wa wakimbizi wanaokimbia migogoro ya silaha.
Somalia: FAO na EU warejesha matumaini kwa wakulima kupitia kilimo cha umwagiliaji
vendredi 27 mars 2026 • Durée 02:28
Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. FAO imekarabati zaidi ya kilomita 300 za mifereji ya umwagiliaji ili kurejesha upatikanaji wa maji katika mashamba na kwa jamii, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha ustahimilivu wa wakazi wa maeneo haya kame nchini Somalia. Wakulima wanasema wameanza kuona matumaini mapya kwani mradi huu wa CLIMB umeboresha maisha yao. Nuur Mukhtar Mohamed ni mmoja wao, anasema uhaba wa maji katika Mto Jordan ulikuwa umeathiri vibaya shughuli za kilimo.Akifafanua anasema, “hapo awali tulikumbana na changamoto kubwa kwa sababu Mto Juba uko chini kuliko mashamba yetu, hali iliyofanya umwagiliaji kuwa mgumu sana. Hata hivyo, mfereji mpya ulioinuliwa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha yetu.”Kwa mujibu wa wakulima wengine, maboresho hayo yameleta unafuu mkubwa katika shughuli za kilimo na maisha ya kila siku. Akiwa shambani, Sadiyo Sheikh Ali, mkulima kutoka kijiji cha Bulo Bartire, anaeleza kwamba,“Kabla ya mfereji huu, maji yalikuwa haba sana kiasi cha kusababisha migogoro baina ya wakulima. Sasa hali imeimarika na tuna matumaini mapya. Tumeanza kupata utulivu wa akili.”Mbali na ukarabati wa mifereji, FAO pia inawapatia wakulima mbegu bora na kuwawezesha kuanzisha vikundi vya Akiba na Mikopo vya Kijiji (VSLA), vinavyosaidia kukuza kipato na kuimarisha mshikamano wa kijamii.Akizungumzia umuhimu wa vikundi hivyo, Yusuf Abdisalam Yusuf, Mkuu wa Kikundi cha Midinimo kutoka Goobweyn, amesema “tumeunda kikundi hiki ili kushirikiana na kusaidiana katika shughuli za kilimo na maisha kwa ujumla, bila kujali ukubwa wa msaada.”Mifereji iliyokarabatiwa sasa inaendelea kufufua matumaini na kuleta fursa mpya za kipato katika eneo la Jubaland. Hata hivyo, wakulima wanasisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongezewa pembejeo, msaada wa kifedha na mafunzo endelevu ili kuhakikisha jamii zinaendelea kustawi.
Baraza la Haki za Binadamu: Tofauti zozote zilizopo kati ya nchi hazitatatuliwa kwa kuwaua wanafunzi
Hii leo jaridani mwenyeji wako Flora Nducha anamulika Mashariki ya Kati, mzozo Sudan Kusini unavyoendelea kuleta machungu kwa raia. Ingawa hivyo kuna habari njema ya jinsi FAO inavyoleta nuru kwa wakulima nchini Somalia kwa kukarabati mifereji ya umwagiliaji. Karibu!===========================Vita huko Mashariki ya Kati vinaendelea leo ikiwa ni siku ya 28, mashambulizi yanasababisha hofu, mateso, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu katika eneo lote. Huko Geneva, Uswisi wanadiplomasia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo wanajadili shambulizi la shule lililotokea Minab, Iran, ambalo limeua zaidi ya watoto 100. Leah Mushi anasimulizi hii ya kusikitisha.Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudani Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Rashid Malekela anatupeleka kufahamu maisha ya wakimbizi huo yapoje?Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.
JIFUNZE KISWAHILI - NENO: NYAPANYAPA
jeudi 26 mars 2026 • Durée
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "NYAPANYAPA" katika muktadha wa uwindaji.Bwana Sigalla anasema "nyapanyapa ni tabia ya mwindaji ambayo anatembea kwa kunyata sana, pole pole ili asisikike wakati anawinda.Anakuwa ananyemelea. Lengo ni kuhakikisha anamsogelea mnyama ama kumshika au kuweza kuwinda mnyama vizuri."
26 MACHI 2026
jeudi 26 mars 2026 • Durée 09:59
Hii leo jaridani tunamulika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), hali Mashariki ya Kati, Amerika ya Kati, kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania na katika kujifunza lugha ya Kiswahili ni uchambuzi wa neno, 'Nyapanyapa.'MUHTASARIMabaraza ya Umoja wa Mataifa lile la Usalama na lile la Haki za Binadamu kwa nyakati tofauti yajadili hali ya usalama na haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Huko Mashariki ya Kati hali ya usalama na kibinadamu yazidi kuwa tete Lebanon na Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea kila uchao.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO azungumzia hali tete ya afya nchini Cuba kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya umeme.MADA KWA KINA: Jinsimafunzo ya kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi yalivyoanza kuonesha matokeo chanya huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania. Mradi ni wa FAO kwa kushirikiana na SMZ.JIFUNZE KISWAHILI- Mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania anafafanua maana ya neno 'Nyapanyapa.'Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Tanzania: FAO na wadau 'wawanoa' maafisa misitu ili kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu
mercredi 25 mars 2026 • Durée 02:52
Nchini Tanzania kunafanyika mafunzo kwa maafisa wa misitu yenye lengo la kulinda misitu, mafunzo yanayotekelezwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa CookFund.Tweet URLMratibu wa Mradi kutoka FAO Diomedes Kalisa akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Msaidizi wa FAO Tanzania, Charles Tulahi, amesema “mafunzo haya yanakuja wakati muafaka kwani maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Misitu yalibeba kaulimbiu, “Misitu na Uchumi.”Amesisitiza kuwa Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 48 za misitu ambayo inachangia zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji ya nishati ya kaya kupitia nishati ya biomasi. Uvunaji haramu wa misitu ni kikwazo“Changamoto za uvunaji haramu, uzalishaji usio endelevu na udhaifu wa utekelezaji wa sheria zinalengwa kupitia mafunzo hayo yatakayojikita katika maeneo matano ya kipaumbele.” Amesema.Ametaja maeneo hayo kuwa ni usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia, tafsiri ya sheria za misitu na marekebisho yake ya 2025, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria. Lengo namba 15 la SDG linavyomulika misituLengo la 15 la Maendeleo Endelevu (SDG15) kuhusu “Uhai juu ya ardhi,” linazingatia kulinda, kurejesha, na kuendeleza usimamizi endelevu wa misitu, kusitisha ukataji miti hovyo, na kurejesha uharibifu wa ardhi ifikapo mwaka 2030. Lengo hili linaelekeza moja kwa moja kusitisha upotevu wa bayonuai na kuimarisha mchango wa misitu katika kunasa hewa ya ukaa, hivyo kusaidia juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.Manufaa ya mafunzoMkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Misitu katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Seleboni Mushi, amesema mafunzo hayo yanayosimamiwa na FAO yanalenga kujenga uwezo wa wakaguzi na wapelelezi wa TFS kutoka maeneo mbalimbali ya nchi katika kudhibiti changamoto zinazoikabili misitu ikiwemo ukataji miti haramu, uvamizi wa misitu, kilimo haramu na uchomaji moto kwenye maeneo ya misitu. “Misitu ni urithi wa taifa na ni muhimu kuilinda kwa ajili ya vizazi vijavyo,” amesema Afisa huyo na hivyo “mafunzo haya yatawapa washiriki maarifa mapya katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ulinzi wa misitu, tafsiri ya sheria na kanuni za misitu, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria.” Amesisitiza kuwa mafunzo haya ni fursa kwa washiriki kujenga mitandao imara ya kitaalamu itakayosaidia ushirikiano na ubadilishanaji wa taarifa katika kuhakikisha misitu ya Tanzania inaendelea kutoa manufaa kwa wote,” amesema Bwana Mushi.
Meli zilizokuwa zikipita Hormuz zilikuwa 129 kwa siku, sasa ni 2 hadi 7 kwa siku: UNCTAD
mercredi 25 mars 2026 • Durée 03:07
Tangu kuanza kwa vita huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran mnamo tarehe 28 Februari na kisha Iran kujibu mashambulizi, wasiwasi umekuwa ukiongezeka kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa nyingine. Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD linafuatilia kwa karibu hali inayoendelea na kutoa takwimu na uchambuzi ili kuzisaidia serikali na wadau wengine waweze kujipanga na kuratibu vyema mambo yao hususan yanayohusiana na usafiri wa baharini.Katikati ya vita hii inayoendelea Mashariki ya Kati kuna suala la mlango bahari wa Hormuz, hili ni eneo muhimu sana lililopo Iran ambako takriban robo ya mafuta yote duniani, meli zake hupita hapo. Bidhaa nyingine muhimu zinazopita hapo ni gesi asilia na mbolea. Ingawa mlango bahari wa Hormuz haujafungwa rasmi, lakini umewekewa vikwazo vikali, huku kukiwa na mashambulizi mengi ya Iran dhidi ya meli tangu vita vilipozuka siku 26 zilizopita. Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD Frida Youssef anaanza kwa kutueleza hali ilivyokuwa kabla ya vita.“Kabla tu ya mzozo, tunapoangalia wastani wa idadi ya meli kwa siku zilizokuwa zikipitia Hormuz, ilikuwa karibu meli 129, 130 na katika wiki mbili zilizopita, ilikuwa karibu meli mbili hadi saba kwa siku.”Kwa lugha nyingine upungufu ni takriban asilimia 95. Je ni maeneo gani yameathirika zaidi? “Usafirishaji wa mbolea unaathirika pamoja na bei ya uzalishaji, kwa mfano, mbolea za nitrojeni ambazo hutegemea sana gesi. Kwa hivyo, hii inabadilisha tena kuwa ni athari kwenye kilimo ambayo baadaye itaonekana kwenye kupanda kwa bei ya chakula.” UN News/Daniel DickinsonKufungwa kwa mlangobahari wa Hormuz kunaathiri biashara kwa kiwango cha kimataifa.Akiendea na tathmini yake Mkuu huyo wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa UNCTAD anasema hivi sasa bei za mafuta zimepanda.“Tumeona bei ya mafuta yanayotumika katika vyombo vya usafiri baharini ikiongezeka maradufu. Hii pia inaathiri gharama ya usafiri, si tu kwasababu bei ya mafuta imepanda bali pia bei, kwa mfano, ya bima. Malipo ya bima ya vita yameongezeka, katika baadhi ya maeneo imeongezeka mara nne.”UNCTAD inaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kwa serikali na wadau kwani vita hii inayoendelea inaathari kwa kila mtu lakini nchi zenye uchumi mdogo ndio zitakazo athirika zaidi kwani zinauwezo mdogo zaidi wa kuvumilia mshtuko huu wa kiuchumi na ndio zitakazohisi athari zake kwa nguvu zaidi. “Inaathiri usafiri, inaathiri nishati, inaathiri chakula na pia inaongeza gharama na upatikanaji ni mgumu. Kwa hivyo, haya yote kwa pamoja yanakuwa na athari kwenye uchumi wa umma katika nchi, pamoja na gharama za maisha kwa kaya.”
Azimio lapitishwa kutambua biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki ni uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu
mercredi 25 mars 2026 • Durée 03:23
Umoja wa Mataifa leo umekuwa na tukio la kumbukizi ya siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlanitiki ambapo nchi 123 wanachama wa Umoja huo wamepitisha azimio lililoandaliwa na mataifa 58 kutambua usafirishaji wa watu wa kiafrika na utumwa kwa misingi ya rangi ya waafrika kuwa uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu. Nchi hizo 123 ni pamoja na zile wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilhali nchi 3 zilizopinga azimio ni Marekani, Israeli na Argentina. Nchi 52 hazikuonesha msimamo wowote. Mwakilishi wa Marekani akizungumza baada ya kupiga kura ya kupinga azimio hilo amesema, "tunalaani makosa yoyote yaliyofanyika kuhusiana na utumwa kuvuka bahari ya Atlantiki, jangwa la Sahara na kwingineko, lakini tumepinga azimio kwa sababu hatuoni msingi wa kulipatia kiwango cha juu hivyo cha hadhi tukio hilo. Na zaidi ya yote kama ni fidia, fidia hiyo atalipwa nani,?" amehoji.Rais wa Ghana aliwasilisha rasimu ya azimio mbele ya Baraza KuuUN/Manuel EliasRais John Mahama wa Ghana akihutubia Baraza Kuu wakati wa siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Rais wa Ghana John Mahama ambaye ni Balozi wa Muungano wa Afrika wa Kuendeleza Hali ya Haki na Fidia. Azimio hilo namba A/80/L.48 limepatiwa jina kutambua usafirishaji wa watu waliokuwa watumwa kutoka Afrika na utumwa kwa msingi wa rangi ya watu wa kiafrika kama mojawapo ya uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu. Azimio hilo lililoandaliwa na mataifa 58 yakiwemo mataifa ya Afrika Mashariki, lina vipengele 16 vya utekelezaji ikiwemo kutambua usafirishaji huo wa watumwa kutoka Afrika kuwa uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu, kurejeshwa kwa mali za kitamaduni kutoka Afrika na zaidi ya yote kulipwa fidia.Kauli ya Rais wa Baraza KuuTukio la kumbukizi lilianza kwa Annalena Baerbock Rais wa Baraza Kuu kuitisha kikao na kisha kuelekea kwenye mimbari kutoa hotuba yake akirejelea simulizi ya mtumwa Oladuk Ekwano kutoka Nigeria ya sasa akielezea machungu ya safari ndani ya meli iliyowabeba.UN/Manuel EliasRais wa Baraza Kuu la UN Annalena Baerbock akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Anasema Makumi ya mamilioni ya wengine kama Egvano walinyang’anywa kutoka kwa familia zao, nchi zao na tamaduni zao, wakafanywa watumwa na kupelekwa kufanya kazi katika nchi za kigeni—kwenye mashamba ya pamba hapa Marekani, na kwenye mashamba ya miwa na kahawa katika makoloni yaliyodhibitiwa na Ulaya. Katika maeneo ambayo leo yanajulikana kama Brazili, Barbados, Jamaica, na maeneo mengine mengi. Wote wakiwa mbali na nyumbani, mbali na familia, mbali na maisha yao.Tunatambua nchi zinazoomba radhi lakini hatua zaidi zahitajikaKwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amerejelea mateso waliyopata mamilioni ya waafrika waliotekwa nyara na kusafirishwa katika hali dhalili na kugeuzwa watumwa barani Amerika. Amesema kumbukumbu pekee haitoshi.Amebainisha kuwa mfumo huo haukuwa tu ukatili wa zamani bali pia ulikuwa msingi wa miundo ya uchumi wa dunia ambayo madhara yake yanaendelea hadi leo katika mfumo wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo na ukosefu wa usawa.UN/Manuel EliasKatibu Mkuu António Guterres akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Hotuba hiyo imesisitiza kuwa kumbukumbu pekee haitoshi. Badala yake, nchi lazima zikabiliane na dhuluma za muda mrefu zinazoendelea kuwaathiri watu wenye asili ya Kiafrika. “Kiini cha juhudi hizo, alisema, ni kutafuta ukweli, haki, na marekebisho, ikiwa ni pamoja na mijadala yenye maana na hatua kuhusu fidia,” amesema Katibu Mkuu. Guterres anasema, “Ndiyo maana Muongo wa Pili wa Kimataifa kwa Watu wenye Asili ya Kiafrika na Muongo wa Fidia wa Muungano wa…
25 MACHI 2025
mercredi 25 mars 2026 • Durée 11:17
Yaliyomo katika Jarida hili la habari za UNKauli za fidia na haki zatawala tukio la kumbukizi ya biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki.UNCTAD: Meli zilizokuwa zikipita Hormuz zilikuwa 129 kwa siku, sasa ni 2 hadi 7 kwa siku.FAO Tanzania na wadau wawanoa maafisa misitu kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu